1 Haleluya.Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote,Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano.
2 Matendo ya BWANA ni makuu,Yafikiriwa sana na wapendezwao nayo.
3 Kazi yake ni heshima na adhama,Na haki yake yakaa milele.
4 Amefanya ukumbusho wa matendo yake ya ajabu;BWANA ni mwenye fadhili na rehema.
5 Amewapa wamchao chakula;Atalikumbuka agano lake milele.
6 Amewajulisha watu wake uwezo wa matendo yake,Kwa kuwapa urithi wa mataifa.
7 Matendo ya mikono yake ni kweli na hukumu,Maagizo yake yote ni amini,
8 Yamethibitika milele na milele,Yamefanywa katika kweli na adili.
9 Amewapelekea watu wake ukombozi,Ameamuru agano lake liwe la milele,Jina lake ni takatifu la kuogopwa.