1 Ee BWANA, hata lini utanisahau, hata milele?Hata lini utanificha uso wako?
2 Hata lini nifanye mashauri nafsini mwangu,Nikihuzunika moyoni mchana kutwa?Hata lini adui yangu atukuke juu yangu?
3 Ee BWANA, Mungu wangu, uangalie, uniitikie;Uyatie nuru macho yangu,Nisije nikalala usingizi wa mauti.
4 Adui yangu asije akasema, Nimemshinda;Watesi wangu wasifurahi ninapoondoshwa.
5 Nami nimezitumainia fadhili zako;Moyo wangu na uufurahie wokovu wako.