1 Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari?Wema wa Mungu upo sikuzote.
2 Ulimi wako watunga madhara,Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila
3 Umependa mabaya kuliko mema,Na uongo kuliko kusema kweli.
4 Umependa maneno yote ya kupoteza watu,Ewe ulimi wenye hila.
5 Lakini Mungu atakuharibu hata milele;Atakuondolea mbali;Atakunyakua hemani mwako;Atakung’oa katika nchi ya walio hai.
6 Nao wenye haki wataona;Wataingiwa na hofu na kumcheka;
7 Kumbe! Huyu ndiye mtu yule,Asiyemfanya Mungu kuwa nguvu zake.Aliutumainia wingi wa mali zake,Na kujifanya hodari kwa madhara yake.
8 Bali mimi ni kama mzeituniUmeao katika nyumba ya Mungu.Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele.