1 Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji.Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu.
2 Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai,Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu?
3 Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku,Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako.
4 Nayakumbuka hayo nikiweka wazi nafsi yangu ndani yangu,Jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano,Na kuwaongoza nyumbani kwa Mungu,Kwa sauti ya furaha na kusifu, mkutano wa sikukuu.
5 Nafsi yangu, kwa nini kuinama,Na kufadhaika ndani yangu?Umtumaini Mungu;Kwa maana nitakuja kumsifu,Aliye afya ya uso wangu,Na Mungu wangu.
6 Nafsi yangu imeinama ndani yangu, kwa hiyo nitakukumbuka,Toka nchi ya Yordani, na Mahermoni, na toka kilima cha Mizari.
7 Kilindi chapigia kelele kilindi kwa sauti ya maboromoko ya maji yako,Gharika zako zote na mawimbi yako yote yamepita juu yangu.
8 Mchana BWANA ataagiza fadhili zake, na usiku wimbo wake utakuwa nami,Naam, maombi kwa Mungu aliye uhai wangu.
9 Nitamwambia Mungu, mwamba wangu, Kwa nini umenisahau?Kwa nini ninakwenda nikihuzunika, adui wakinionea?
10 Watesi wangu hunitukana mithili ya kuniponda mifupa yangu,Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako?