1 Enyi watu wote, pigeni makofi,Mpigieni Mungu kelele kwa Sauti ya shangwe.
2 Kwa kuwa BWANA Aliye juu, mwenye kuogofya,Ndiye mfalme mkuu juu ya dunia yote.
3 Atawatiisha watu wa nchi chini yetu,Na mataifa chini ya miguu yetu.
4 Atatuchagulia urithi wetu,Fahari ya Yakobo ambaye alimpenda.
5 Mungu amepaa kwa kelele za shangwe,BWANA kwa sauti ya baragumu.
6 Mwimbieni Mungu, naam, imbeni;Mwimbieni mfalme wetu, naam, imbeni.
7 Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote,Imbeni kwa akili.
8 Mungu awamiliki mataifa,Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu.