1 Mungu, uisikie sauti yangu katika malalamiko yangu;Unilinde uhai wangu na hofu ya adui.
2 Utanificha mbali na shauri la siri la watenda mabaya,Mbali na ghasia ya watu wafanyao maovu;
3 Waliounoa ulimi wao kama upanga,Wameielekeza mishale yao, maneno ya uchungu,
4 Wapate kumpiga mkamilifu faraghani,Kwa ghafula humpiga wala hawaogopi.
5 Walijifanya hodari katika jambo baya;Hushauriana juu ya kutega mitego;Husema, Ni nani atakayeiona?
6 Hutunga maovu; husema, Tumefanya shauri kamili;Na mawazo ya ndani ya kila mmoja wao,Na moyo wake, huwa siri kabisa.
7 Kwa hiyo Mungu atawapiga shabaha,Kwa mshale mara watapigwa.
8 Ndivyo watakavyokwazwa,Ulimi wao wenyewe ukishindana nao.Wote wawaonao watatikisa kichwa.
9 Na watu wote wataogopa,Wataitangaza kazi ya Mungu,Na kuyafahamu matendo yake.