1 Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya BWANA,Dunia na wote wakaao ndani yake.
2 Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari,Na juu ya mito ya maji aliithibitisha.
3 Ni nani atakayepanda katika mlima wa BWANA?Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake?
4 Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe,Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili,Wala hakuapa kwa hila.
5 Atapokea baraka kwa BWANA,Na haki kwa Mungu wa wokovu wake.
6 Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao,Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.
7 Inueni vichwa vyenu, enyi malango,Inukeni, enyi malango ya milele,Mfalme wa utukufu apate kuingia.
8 Ni nani Mfalme wa utukufu?BWANA mwenye nguvu, hodari,BWANA hodari wa vita.
9 Inueni vichwa vyenu, enyi malango,Naam, viinueni, enyi malango ya milele,Mfalme wa utukufu apate kuingia.