1 Ee Mungu, ukisikie kilio changu,Uyasikilize maombi yangu.
2 Toka mwisho wa nchi nitakulilia nikizimia moyo,Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda.
3 Kwa maana ulikuwa kimbilio langu,Ngome yenye nguvu adui asinipate.
4 Nitakaa katika hema yako milele,Nitaikimbilia sitara ya mbawa zako
5 Maana Wewe, Mungu, umezisikia nadhiri zangu.Umewapa urithi wao waliogopao jina lako.
6 Utaziongeza siku za mfalme,Miaka yake itakuwa kama vizazi vingi.
7 Atakaa mbele za Mungu milele,Ziagize fadhili na kweli zimhifadhi.