1 Neno la BWANA kwa Bwana wangu,Uketi mkono wangu wa kuume,Hata niwafanyapo adui zakoKuwa chini ya miguu yako.
2 BWANA atainyosha toka SayuniFimbo ya nguvu zako.Uwe na enzi kati ya adui zako;
3 Watu wako wanajitoa kwa hiari,Siku ya uwezo wako;Kwa uzuri wa utakatifu,Tokea tumbo la asubuhi,Unao umande wa ujana wako.
4 BWANA ameapa,Wala hataghairi,Ndiwe kuhani hata milele,Kwa mfano wa Melkizedeki.
5 Bwana yu mkono wako wa kuume;Ataseta wafalme,Siku ya ghadhabu yake.
6 Atahukumu kati ya mataifa,Ataijaza nchi mizoga;Ataseta kichwa katika nchi nyingi.