Zab. 136 SUV

Uumbaji wa Mungu na Matukio ya Kihistoria

1 Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

2 Mshukuruni Mungu wa miungu;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

3 Mshukuruni Bwana wa mabwana;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

4 Yeye peke yake afanya maajabu makuu;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

5 Yeye aliyefanya mbingu kwa fahamu zake;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

6 Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

7 Yeye aliyefanya mianga mikubwa;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

8 Jua litawale mchana;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

9 Mwezi na nyota zitawale usiku;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

10 Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wa kwanza wao;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

11 Akawatoa Waisraeli katikati yao;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

12 Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

13 Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

14 Akawavusha Israeli katikati yake;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

15 Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

16 Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

17 Yeye aliyewapiga wafalme wakuu;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

18 Akawaua wafalme mashuhuri;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

19 Sihoni, mfalme wa Waamori;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

20 Na Ogu, mfalme wa Bashani;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

21 Akaitoa nchi yao iwe urithi;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

22 Urithi wa Israeli mtumishi wake;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

23 Aliyetukumbuka katika unyonge wetu;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

24 Akatuokoa na watesi wetu;Kwa maana fadhili zake ni za milele.

25 Kila chenye mwili akipa chakula chake;Kwa maana fadhili zake ni za milele.