1 Ee Bwana, unihukumu, unitetee kwa taifa lisilo haki,Uniokoe na mtu wa hila asiye haki.
2 Kwa kuwa Wewe ndiwe Mungu uliye nguvu zangu; kwa nini umenitupa?Kwa nini ninakwenda nikihuzunika, adui wakinionea?
3 Niletewe nuru yako na kweli yako ziniongoze,Zinifikishe kwenye mlima wako mtakatifu na hata maskani yako.
4 Hivyo nitakwenda madhabahuni kwa Mungu, kwa Mungu aliyefuraha yangu na shangwe yangu;Nitakusifu kwa kinubi, Ee MUNGU, Mungu wangu.