1 Ee BWANA, nitakuita Wewe, mwamba wangu,Usiwe kwangu kama kiziwi.Nisije nikafanana nao washukao shimoni,Ikiwa umeninyamalia.
2 Uisikie sauti ya dua yangu nikuombapo,Nikipainulia patakatifu pako mikono yangu.
3 Usinikokote pamoja na wasio haki,Wala pamoja na watenda maovu.Wawaambiao jirani zao maneno ya amani,Lakini mioyoni mwao mna madhara.
4 Uwape sawasawa na vitendo vyao,Na kwa kadiri ya ubaya wa kufanya kwao,Uwape sawasawa na kazi ya mikono yao,Uwalipe stahili zao.
5 Maana hawazifahamu kazi za BWANA,Wala matendo ya mikono yake.Atawavunja wala hatawajenga;
6 Na ahimidiwe BWANA.Maana ameisikia sauti ya dua yangu;
7 BWANA ni nguvu zangu na ngao yangu.Moyo wangu umemtumaini,Nami nimesaidiwa;Basi, moyo wangu unashangilia,Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.
8 BWANA ni nguvu za watu wake,Naye ni ngome ya wokovu kwa masihi wake.