1 Heri kila mtu amchaye BWANA,Aendaye katika njia yake.
2 Taabu ya mikono yako hakika utaila;Utakuwa heri, na kwako kwema.
3 Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao,Vyumbani mwa nyumba yako.Wanao kama miche ya mizeituniWakiizunguka meza yako.
4 Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye BWANA.
5 BWANA akubariki toka Sayuni;Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako;