1 Haleluya.Heri mtu yule amchaye BWANA,Apendezwaye sana na maagizo yake.
2 Wazao wake watakuwa hodari duniani;Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa.
3 Nyumbani mwake mna utajiri na mali,Na haki yake yakaa milele.
4 Nuru huwazukia wenye adili gizani;Ana fadhili na huruma na haki.
5 Heri atendaye fadhili na kukopesha;Atengenezaye mambo yake kwa haki.
6 Kwa maana hataondoshwa kamwe;Mwenye haki atakumbukwa milele.
7 Hataogopa habari mbaya;Moyo wake u imara ukimtumaini BWANA.
8 Moyo wake umethibitika hataogopa,Hata awaone watesi wake wameshindwa.
9 Amekirimu, na kuwapa maskini,Haki yake yakaa milele,Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.