1 Heri aliyesamehewa dhambi,Na kusitiriwa makosa yake.
2 Heri BWANA asiyemhesabia upotovu,Ambaye rohoni mwake hamna hila.
3 Niliponyamaza mifupa yangu ilichakaaKwa kuugua kwangu mchana kutwa.
4 Kwa maana mchana na usikuMkono wako ulinilemea.Jasho langu likakauka hata nikawaKama nchi kavu wakati wa kaskazi.
5 Nalikujulisha dhambi yangu,Wala sikuuficha upotovu wangu.Nalisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA,Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.
6 Kwa hiyo kila mtu mtauwaAkuombe wakati unapopatikana.Hakika maji makuu yafurikapo,Hayatamfikia yeye.
7 Ndiwe sitara yangu, utanihifadhi na mateso,Utanizungusha nyimbo za wokovu.
8 Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea;Nitakushauri, jicho langu likikutazama.
9 Msiwe kama farasi wala nyumbu,Walio hawana akili.Kwa matandiko ya lijamu na hatamuSharti kuwazuia hao, au hawatakukaribia.
10 Naye mtu mwovu ana mapigo mengi,Bali amtumainiye BWANA fadhili zitamzunguka.