1 Mungu na atufadhili na kutubariki,Na kutuangazia uso wake.
2 Njia yake ijulike duniani,Wokovu wake katikati ya mataifa yote.
3 Watu na wakushukuru, Ee Mungu,Watu wote na wakushukuru.
4 Mataifa na washangilie,Naam, waimbe kwa furaha,Maana kwa haki utawahukumu watu,Na kuwaongoza mataifa walioko duniani.
5 Watu na wakushukuru, Ee Mungu,Watu wote na wakushukuru.
6 Nchi imetoa mazao yakeMUNGU, Mungu wetu, ametubariki.