1 Ee BWANA, nimekuita, unijie hima,Uisikie sauti yangu nikuitapo.
2 Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba,Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.
3 Ee BWANA, uweke mlinzi kinywani pangu,Mngojezi mlangoni pa midomo yangu.
4 Usiuelekeze moyo wangu kunako jambo baya,Nisiyazoelee matendo yasiyofaa,Pamoja na watu watendao maovu;Wala nisile vyakula vyao vya anasa.
5 Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili;Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani;Kichwa changu kisikatae,Maana siachi kusali kati ya mabaya yao.
6 Makadhi wao wakiangushwa kando ya genge,Watayasikia maneno yangu, maana ni matamu.
7 Kama kupasua kuni na kuzichanja juu ya nchi,Ndivyo ilivyo mifupa yetu mdomoni pa kuzimu.
8 Macho yangu yanakuelekea Wewe, MUNGU Bwana,Nimekukimbilia Wewe, usiniache nafsi yangu.
9 Unilinde na mtego walionitegea,Na matanzi yao watendao maovu.