1 BWANA ametamalaki, amejivika adhama,BWANA amejivika, na kujikaza nguvu.Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;
2 Kiti chako kimekuwa thabiti tokea zamani;Wewe ndiwe uliye tangu milele.
3 Ee BWANA, mito imepaza,Mito imepaza sauti zake,Mito imepaza uvumi wake.
4 Kupita sauti ya maji mengi, maji makuu,Kupita mawimbi ya bahari yaumkayo,BWANA Aliye juu ndiye mwenye ukuu.