1 Haleluya.Enyi watumishi wa BWANA, sifuni,Lisifuni jina la BWANA.
2 Jina la BWANA lihimidiweTangu leo na hata milele.
3 Toka maawio ya jua hata machweo yakeJina la BWANA husifiwa.
4 BWANA ni mkuu juu ya mataifa yote,Na utukufu wake ni juu ya mbingu.
5 Ni nani aliye mfano wa BWANA,Mungu wetu aketiye juu;
6 Anyenyekeaye kutazama,Mbinguni na duniani?
7 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,Na kumpandisha maskini kutoka jaani.
8 Amketishe pamoja na wakuu,Pamoja na wakuu wa watu wake.