1 Ee BWANA, utege sikio lako unijibu,Maana mimi ni maskini na mhitaji
2 Unihifadhi nafsi yangu,Maana mimi ni mcha Mungu.Wewe uliye Mungu wangu,Umwokoe mtumishi wako anayekutumaini.
3 Wewe, Bwana, unifadhili,Maana nakulilia Wewe mchana kutwa.
4 Uifurahishe nafsi ya mtumishi wako,Maana nafsi yangu nakuinulia Wewe, Bwana.
5 Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema,Umekuwa tayari kusamehe,Na mwingi wa fadhili,Kwa watu wote wakuitao.
6 Ee BWANA, uyasikie maombi yangu;Uisikilize sauti ya dua zangu.
7 Siku ya mateso yangu nitakuita,Kwa maana utaniitikia.
8 Katikati ya miungu hakuna kama Wewe, Bwana,Wala matendo mfano wa matendo yako.
9 Mataifa yote uliowafanya watakuja;Watakusujudia Wewe, Bwana,Watalitukuza jina lako;
10 Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu,Wewe ndiwe mfanya miujiza,Ndiwe Mungu peke yako.
11 Ee BWANA, unifundishe njia yako;Nitakwenda katika kweli yako;Moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako;
12 Nitakusifu Wewe, Bwana, Mungu wangu,Kwa moyo wangu wote,Nitalitukuza jina lako milele.
13 Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana;Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu.
14 Ee Mungu, wenye kiburi wamenishambulia;Mkutano wa wakatili wamenitafuta roho.Wala hawakukuweka WeweMbele ya macho yao.
15 Lakini Wewe, Bwana,U Mungu wa rehema na neema,Mvumilivu, mwingi wa fadhili na kweli.
16 Unielekee na kunifadhili mimi;Mpe mtumishi wako nguvu zako,Umwokoe mwana wa mjakazi wako.