1 Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi,Israeli na aseme sasa,
2 Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi,Wanadamu walipotushambulia.
3 Papo hapo wangalitumeza hai,Hasira yao ilipowaka juu yetu
4 Papo hapo maji yangalitugharikisha,Mto ungalipita juu ya roho zetu;
5 Papo hapo yangalipita juu ya nafsi zetuMaji yafurikayo.
6 Na ahimidiwe BWANA;Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao.
7 Nafsi yetu imeokoka kama ndegeKatika mtego wa wawindaji,Mtego umevunjika, nasi tumeokoka.