1 Kwa sauti yangu nitamlilia BWANA,Kwa sauti yangu nitamwomba BWANA dua.
2 Nitafunua mbele zake malalamiko yangu,Shida yangu nitaitangaza mbele zake.
3 Nilipozimia roho uliyajua mapito yangu;Katika njia niendayo wamenifichia mtego.
4 Utazame mkono wa kuume ukaone,Kwa maana sina mtu anijuaye.Makimbilio yamenipotea,Hakuna wa kunitunza roho.
5 BWANA, nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu,Fungu langu katika nchi ya walio hai.
6 Ukisikilize kilio changu,Kwa maana nimedhilika sana.Uniponye nao wanaonifuatia,Kwa maana wao ni hodari kuliko mimi.