1 Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake kwa kimya,Wokovu wangu hutoka kwake.
2 Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu,Ngome yangu, sitatikisika sana.
3 Hata lini mtamshambulia mtu,Mpate kumwua ninyi nyote pamoja?Kama ukuta unaoinama,Kama kitalu kilicho tayari kuanguka,
4 Hufanya shauri kumwangusha tu katika cheo chake;Huufurahia uongo.Kwa kinywa chao hubariki;Kwa moyo wao hulaani.
5 Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa kimya.Tumaini langu hutoka kwake.
6 Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu,Ngome yangu, sitatikisika sana.
7 Kwa Mungu wokovu wangu,Na utukufu wangu;Mwamba wa nguvu zangu,Na kimbilio langu ni kwa Mungu.
8 Enyi watu, mtumainini sikuzote,Ifunueni mioyo yenu mbele zake;Mungu ndiye kimbilio letu.
9 Hakika binadamu ni ubatili,Na wenye cheo ni uongo,Katika mizani huinuka;Wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili.
10 Msiitumainie dhuluma,Wala msijivune kwa unyang’anyi;Mali izidipo msiiangalie sana moyoni.
11 Mara moja amenena Mungu;Mara mbili nimeyasikia haya,Ya kuwa nguvu zina Mungu,