1 BWANA ametamalaki, nchi na ishangilie,Visiwa vingi na vifurahi.
2 Mawingu na giza vyamzunguka,Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake.
3 Moto hutangulia mbele zake,Nao huwateketeza watesi wake pande zote.
4 Umeme wake uliuangaza ulimwengu,Nchi ikaona ikatetemeka.
5 Milima iliyeyuka kama nta mbele za BWANA,Mbele za Bwana wa dunia yote.
6 Mbingu zimetangaza haki yake,Na watu wote wameuona utukufu wake.
7 Na waaibishwe wote waabuduo sanamu,Wajivunao kwa vitu visivyofaa;Enyi miungu yote, msujuduni Yeye.
8 Sayuni imesikia na kufurahi,Binti za Yuda walishangilia,Kwa sababu ya hukumu zako, Ee BWANA.
9 Maana Wewe, BWANA, ndiwe Uliye juu,Juu sana kuliko nchi yote;Umetukuka sana juu ya miungu yote.
10 Enyi mmpendao BWANA, uchukieni uovu;Huwalinda nafsi zao watauwa wake,Na kuwaokoa na mkono wa wasio haki.
11 Nuru imemzukia mwenye haki,Na furaha wanyofu wa moyo.