1 Mwimbieni BWANA wimbo mpya,Kwa maana ametenda mambo ya ajabu.Mkono wa kuume wake mwenyewe,Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu.
2 BWANA ameufunua wokovu wake,Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake.
3 Amezikumbuka rehema zake,Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli.Miisho yote ya dunia imeuonaWokovu wa Mungu wetu.
4 Mshangilieni BWANA, nchi yote,Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi.
5 Mwimbieni BWANA zaburi kwa kinubi,Kwa kinubi na sauti ya zaburi.
6 Kwa panda na sauti ya baragumu.Shangilieni mbele za Mfalme, BWANA.
7 Bahari na ivume na vyote viijazavyo,Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake.
8 Mito na ipige makofi,Milima na iimbe pamoja kwa furaha.