1 BWANA ndiye mchungaji wangu,Sitapungukiwa na kitu.
2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza,Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
3 Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongozaKatika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,Sitaogopa mabaya;Kwa maana Wewe upo pamoja nami,Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
5 Waandaa meza mbele yangu,Machoni pa watesi wangu.Umenipaka mafuta kichwani pangu,Na kikombe changu kinafurika.