1 Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni,Ambao hautatikisika, wakaa milele.
2 Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu,Ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake,Tangu sasa na hata milele.
3 Kwa maana fimbo ya udhalimuHaitakaa juu ya fungu la wenye haki;Wenye haki wasije wakainyoshaMikono yao kwenye upotovu.
4 Ee BWANA, uwatendee mema walio wema,Nao walio wanyofu wa moyo.