1 Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi,Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe.Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako,Hata misiba hii itakapopita.
2 Nitamwita MUNGU Aliye juu,Mungu anitimiziaye mambo yangu.
3 Atapeleka toka mbinguni na kuniokoa,Atukanapo yule atakaye kunimeza.Mungu atazipelekaFadhili zake na kweli yake
4 Nafsi yangu i kati ya simba,Nitastarehe kati yao waliowaka moto.Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale,Na ndimi zao ni upanga mkali.
5 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.
6 Wameweka wavu ili kuninasa miguu;Nafsi yangu imeinama;Wamechimba shimo mbele yangu;Wametumbukia ndani yake!
7 Ee Mungu, moyo wangu u thabiti,Moyo wangu u thabiti.Nitaimba, nitaimba zaburi,
8 Amka, utukufu wangu.Amka, kinanda na kinubi,Nitaamka alfajiri.
9 Ee Bwana, nitakushukuru kati ya watu,Nitakuimbia zaburi kati ya mataifa.
10 Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni,Na uaminifu wako hata mawinguni.