1 Ee BWANA, toka vilindini nimekulilia.
2 Bwana, uisikie sauti yangu.Masikio yako na yaisikilizeSauti ya dua zangu.
3 BWANA, kama Wewe ungehesabu maovu,Ee Bwana, nani angesimama?
4 Lakini kwako kuna msamaha,Ili Wewe uogopwe.
5 Nimemngoja BWANA, roho yangu imengoja,Na neno lake nimelitumainia.
6 Nafsi yangu inamngoja Bwana,Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi,Naam, walinzi waingojao asubuhi.
7 Ee Israeli, umtarajie BWANA;Maana kwa BWANA kuna fadhili,Na kwake kuna ukombozi mwingi.