1 BWANA alipowarejeza mateka wa Sayuni,Tulikuwa kama waotao ndoto.
2 Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko,Na ulimi wetu kelele za furaha.Ndipo waliposema katika mataifa,BWANA amewatendea mambo makuu.
3 BWANA alitutendea mambo makuu,Tulikuwa tukifurahi.
4 Ee BWANA, uwarejeze watu wetu waliofungwa,Kama vijito vya Kusini.
5 Wapandao kwa machoziWatavuna kwa kelele za furaha.