1 BWANA, ni nani atakayekaaKatika hema yako?Ni nani atakayefanya maskani yakeKatika kilima chako kitakatifu?
2 Ni mtu aendaye kwa ukamilifu,Na kutenda haki.Asemaye kweli kwa moyo wake,
3 Asiyesingizia kwa ulimi wake.Wala hakumtenda mwenziwe mabaya,Wala hakumsengenya jirani yake.
4 Machoni pake mtu asiyefaa hudharauliwa,Bali huwaheshimu wamchao BWANAIngawa ameapa kwa hasara yake,Hayabadili maneno yake.