1 Haleluya.Msifuni Mungu katika patakatifu pake;Msifuni katika anga la uweza wake.
2 Msifuni kwa matendo yake makuu;Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu;Msifuni kwa kinanda na kinubi;
4 Msifuni kwa matari na kucheza;Msifuni kwa zeze na filimbi;
5 Msifuni kwa matoazi yaliayo;Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
6 Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA.Haleluya.