1 Ee BWANA, kutukuza usitutukuze sisi,Bali ulitukuze jina lako,Kwa ajili ya fadhili zako,Kwa ajili ya uaminifu wako.
2 Kwa nini mataifa kusema,Yuko wapi Mungu wao?
3 Lakini Mungu wetu yuko mbinguni,Alitakalo lote amelitenda.
4 Sanamu zao ni fedha na dhahabu,Kazi ya mikono ya wanadamu.
5 Zina vinywa lakini hazisemi,Zina macho lakini hazioni,
6 Zina masikio lakini hazisikii,Zina pua lakini hazisikii harufu,
7 Mikono lakini hazishiki, miguu lakini haziendi,Wala hazitoi sauti kwa koo zake.
8 Wazifanyao watafanana nazo,Kila mmoja anayezitumainia.
9 Enyi Israeli, mtumainini BWANA;Yeye ni msaada wao na ngao yao.
10 Enyi mlango wa Haruni, mtumainini BWANA;Yeye ni msaada wao na ngao yao.
11 Enyi mmchao BWANA, mtumainini BWANA;Yeye ni msaada wao na ngao yao.
12 BWANA ametukumbuka,Naye atatubariki sisi.Ataubariki mlango wa Israeli,Ataubariki mlango wa Haruni,
13 Atawabariki wamchao BWANA,Wadogo kwa wakubwa.
14 BWANA na awaongeze ninyi,Ninyi na watoto wenu.
15 Na mbarikiwe ninyi na BWANA,Aliyezifanya mbingu na nchi.
16 Mbingu ni mbingu za BWANA,Bali nchi amewapa wanadamu.
17 Sio wafu wamsifuo BWANA,Wala wo wote washukao kwenye kimya;