1 Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu,Israeli na aseme sasa,
2 Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu,Lakini hawakuniweza.
3 Wakulima wamelima mgongoni mwangu,Wamefanya mirefu mifuo yao.
4 BWANA ndiye mwenye haki,Amezikata kamba zao wasio haki.
5 Na waaibishwe, warudishwe nyuma,Wote wanaoichukia Sayuni.
6 Na wawe kama majani ya dariniYanyaukayo kabla hayajamea.
7 Ambayo mvunaji haujazi mkono wake,Wala mfunga miganda kifua chake.