Zab. 45 SUV

Wimbo wa Arusi ya Kifalme

1 Moyo wangu umefurika kwa neno jema,Mimi nasema niliyomfanyizia mfalme;Ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi mstadi.

2 Wewe u mzuri sana kuliko wanadamu;Neema imemiminiwa midomoni mwako,Kwa hiyo Mungu amekubariki hata milele.

3 Jifungie upanga wako pajani, wewe uliye hodari,Utukufu ni wako na fahari ni yako.

4 Katika fahari yako usitawi uendeleeKwa ajili ya kweli na upole na hakiNa mkono wako wa kuumeUtakufundisha mambo ya kutisha.

5 Mishale yako ni mikali, watu huanguka chini yako;Imo mioyoni mwa adui za mfalme.

6 Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele,Fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.

7 Umeipenda haki;Umeichukia dhuluma.Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekupaka mafuta,Mafuta ya furaha kuliko wenzako.

8 Mavazi yako yote hunukia manemaneNa udi na mdalasini.Katika majumba ya pembeVinubi vimekufurahisha.

9 Binti za wafalme wamoMiongoni mwa akina bibi wako wastahiki.Mkono wako wa kuume amesimama malkiaAmevaa dhahabu ya Ofiri.

10 Sikia, binti, utazame, utege sikio lako,Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako.

11 Naye mfalme atautamani uzuri wako,Maana ndiye bwana wako, nawe umsujudie.

12 Na binti Tiro analeta kipawa chake,Nao matajiri wa watu watajipendekeza kwako.

13 Binti mfalme yumo ndani ana fahari tupu,Mavazi yake ni ya nyuzi za dhahabu.

14 Atapelekwa kwa mfalmeNa mavazi yaliyofumwa kwa uzuri.Wanawali wenzake wanaomfuata,Watapelekwa kwako.

15 Watapelekwa kwa furaha na shangwe,Na kuingia katika nyumba ya mfalme.

16 Badala ya baba zako watakuwapo watoto wako,Utawafanya kuwa wakuu katika nchi zote.