1 Ee BWANA, nitakutukuza kwa maana umeniinua,Wala hukuwafurahisha adui zangu juu yangu.
2 Ee BWANA, Mungu wangu,Nalikulilia ukaniponya.
3 Umeniinua nafsi yangu,Ee BWANA, kutoka kuzimu.Umenihuisha na kunitoaMiongoni mwao washukao shimoni.
4 Mwimbieni BWANA zaburi,Enyi watauwa wake.Na kufanya shukrani.Kwa kumbukumbu la utakatifu wake.
5 Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo,Katika radhi yake mna uhai.Huenda kilio huja kukaa usiku,Lakini asubuhi huwa furaha.
6 Nami nilipofanikiwa nalisema,Sitaondoshwa milele.
7 BWANA, kwa radhi yakoWewe uliuimarisha mlima wangu.Uliuficha uso wako,Nami nikafadhaika.
8 Ee BWANA, nalikulilia Wewe,Naam, kwa BWANA naliomba dua.
9 Mna faida gani katika damu yanguNishukapo shimoni?Mavumbi yatakusifu?Yataitangaza kweli yako?
10 Ee BWANA, usikie, unirehemu,BWANA, uwe msaidizi wangu.
11 Uligeuza matanga yangu kuwa machezo;Ulinivua gunia, ukanivika furaha.