1 Msingi wake upoJuu ya milima mitakatifu.
2 BWANA ayapenda malango ya SayuniKuliko maskani zote za Yakobo.
3 Umetajwa kwa mambo matukufu,Ee Mji wa Mungu.
4 Nitataja Rahabu na BabeliMiongoni mwao wanaonijua.Tazama Filisti, na Tiro, na Kushi;Huyu alizaliwa humo.
5 Naam, mintarafu Sayuni itasemwa,Huyu na huyu alizaliwa humo.Na Yeye Aliye juuAtaufanya imara.
6 BWANA atahesabu, awaandikapo mataifa,Huyu alizaliwa humo.