1 Ee BWANA, kwa nini wasimama mbali?Kwani kujificha nyakati za shida?
2 Kwa kiburi chake asiye haki mnyonge anafuatiwa kwa ukali;Na wanaswe kwa hila zizo hizo walizoziwaza.
3 Maana mdhalimu hujisifia tamaa ya nafsi yake,Na mwenye choyo humkana BWANA na kumdharau.
4 Mdhalimu kwa kiburi cha uso wakeAsema, Hatapatiliza.Jumla ya mawazo yake ni, Hakuna Mungu;