5 Njia zake ni thabiti kila wakati.Hukumu zako ziko juu asizione,Adui zake wote awafyonya.
6 Asema moyoni mwake, Sitaondoshwa,Kizazi baada ya kizazi sitakuwamo taabuni.
7 Kinywa chake kimejaa laana,Na hila na dhuluma.Chini ya ulimi wake kuna madhara na uovu,
8 Hukaa katika maoteo ya vijiji.Mahali pa siri humwua asiye na hatia,Macho yake humvizia mtu duni.
9 Huotea faraghani kama simba pangoni,Huotea amkamate mtu mnyonge.Naam, humkamata mtu mnyonge,Akimkokota wavuni mwake.
10 Hujikunyata na kuinama;Watu duni huanguka kwa nguvu zake.
11 Asema moyoni mwake, Mungu amesahau,Auficha uso wake, haoni kamwe.