1 Rehema na hukumu nitaziimba,Ee BWANA, nitakuimbia zaburi.
2 Nitaiangalia njia ya unyofu;Utakuja kwangu lini?Nitakwenda kwa unyofu wa moyoNdani ya nyumba yangu.
3 Sitaweka mbele ya macho yanguNeno la uovu.Kazi yao waliopotoka naichukia,Haitaambatana nami.
4 Moyo wa ukaidi utaondoka kwangu,Lililo ovu sitalijua.
5 Amsingiziaye jirani yake kwa siri,Huyo nitamharibu.Mwenye macho ya kiburi na moyo wa majivuno,Huyo sitavumilia naye.
6 Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi,Hao wakae nami.Yeye aendaye katika njia kamilifu,Ndiye atakayenitumikia.
7 Hatakaa ndani ya nyumba yanguMtu atendaye hila.Asemaye uongo hatathibitikaMbele ya macho yangu.