1 Ee BWANA, usikie kuomba kwangu,Kilio changu kikufikie.
2 Usinifiche uso wako siku ya shida yangu,Unitegee sikio lako, siku niitapo unijibu upesi.
3 Maana siku zangu zinatoweka kama moshi,Na mifupa yangu inateketea kama kinga.
4 Moyo wangu umepigwa kama majani na kukauka,Naam, ninasahau kula chakula changu.