1 Ee BWANA, usikie kuomba kwangu,Kilio changu kikufikie.
2 Usinifiche uso wako siku ya shida yangu,Unitegee sikio lako, siku niitapo unijibu upesi.
3 Maana siku zangu zinatoweka kama moshi,Na mifupa yangu inateketea kama kinga.
4 Moyo wangu umepigwa kama majani na kukauka,Naam, ninasahau kula chakula changu.
5 Kwa ajili ya sauti ya kuugua kwanguMifupa yangu imegandamana na nyama yangu.
6 Nimekuwa kama mwari nyuni wa jangwani,Na kufanana na bundi wa mahameni.
7 Nakesha, tena nimekuwa kama shomoroAliye peke yake juu ya nyumba.