4 Moyo wangu umepigwa kama majani na kukauka,Naam, ninasahau kula chakula changu.
5 Kwa ajili ya sauti ya kuugua kwanguMifupa yangu imegandamana na nyama yangu.
6 Nimekuwa kama mwari nyuni wa jangwani,Na kufanana na bundi wa mahameni.
7 Nakesha, tena nimekuwa kama shomoroAliye peke yake juu ya nyumba.
8 Adui zangu wananilaumu mchana kutwa;Wanaonichukia kana kwamba wana wazimuHuapa kwa kunitaja mimi.
9 Maana nimekula majivu kama chakula,Na kukichanganya kinywaji changu na machozi.
10 Kwa sababu ya ghadhabu yako na hasira yako;Maana umeniinua na kunitupilia mbali.