1 Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.Naam, vyote vilivyo ndani yanguVilihimidi jina lake takatifu.
2 Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA,Wala usizisahau fadhili zake zote.
3 Akusamehe maovu yako yote,Akuponya magonjwa yako yote,
4 Aukomboa uhai wako na kaburi,Akutia taji ya fadhili na rehema,
5 Aushibisha mema uzee wako,Ujana wako ukarejezwa kama tai;