2 Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA,Wala usizisahau fadhili zake zote.
3 Akusamehe maovu yako yote,Akuponya magonjwa yako yote,
4 Aukomboa uhai wako na kaburi,Akutia taji ya fadhili na rehema,
5 Aushibisha mema uzee wako,Ujana wako ukarejezwa kama tai;
6 BWANA ndiye afanyaye mambo ya haki,Na hukumu kwa wote wanaoonewa.
7 Alimjulisha Musa njia zake,Wana wa Israeli matendo yake.
8 BWANA amejaa huruma na neema,Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.