18 Milima mirefu ndiko waliko mbuzi wa mwitu,Na magenge ni kimbilio la wibari.
19 Aliufanya mwezi kwa ajili ya nyakati,Jua latambua kuchwa kwake.
20 Wewe hufanya giza, kukawa usiku,Ndipo atambaapo kila mnyama wa mwitu.
21 Wana-simba hunguruma wakitaka mawindo,Ili kutafuta chakula chao kwa Mungu.
22 Jua lachomoza, wanakwenda zao,Na kujilaza mapangoni mwao.
23 Mwanadamu atoka kwenda zake kazini,Na kwenye utumishi wake mpaka jioni.
24 Ee BWANA, jinsi yalivyo mengi matendo yako!Kwa hekima umevifanya vyote pia.Dunia imejaa mali zako.