21 Wana-simba hunguruma wakitaka mawindo,Ili kutafuta chakula chao kwa Mungu.
22 Jua lachomoza, wanakwenda zao,Na kujilaza mapangoni mwao.
23 Mwanadamu atoka kwenda zake kazini,Na kwenye utumishi wake mpaka jioni.
24 Ee BWANA, jinsi yalivyo mengi matendo yako!Kwa hekima umevifanya vyote pia.Dunia imejaa mali zako.
25 Bahari iko kule, kubwa na upana,Ndimo mlimo viendavyo visivyohesabika,Viumbe hai vidogo kwa vikubwa.
26 Ndimo zipitamo merikebu,Ndimo alimo lewiathani uliyemwumba acheze humo.
27 Hao wote wanakungoja Wewe,Uwape chakula chao kwa wakati wake.