26 Ndimo zipitamo merikebu,Ndimo alimo lewiathani uliyemwumba acheze humo.
27 Hao wote wanakungoja Wewe,Uwape chakula chao kwa wakati wake.
28 Wewe huwapa,Wao wanakiokota;Wewe waukunjua mkono wako,Wao wanashiba mema;
29 Wewe wauficha uso wako,Wao wanafadhaika;Waiondoa pumzi yao, wanakufa,Na kuyarudia mavumbi yao,
30 Waipeleka roho yako, wanaumbwa,Nawe waufanya upya uso wa nchi.
31 Utukufu wa BWANA na udumu milele;BWANA na ayafurahie matendo yake.
32 Aitazama nchi, inatetemeka;Aigusa milima, inatoka moshi.