29 Wewe wauficha uso wako,Wao wanafadhaika;Waiondoa pumzi yao, wanakufa,Na kuyarudia mavumbi yao,
30 Waipeleka roho yako, wanaumbwa,Nawe waufanya upya uso wa nchi.
31 Utukufu wa BWANA na udumu milele;BWANA na ayafurahie matendo yake.
32 Aitazama nchi, inatetemeka;Aigusa milima, inatoka moshi.
33 Nitamwimbia BWANA maadamu ninaishi;Nitamshangilia Mungu wangu nikiwa hai;
34 Kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake;Mimi nitamfurahia BWANA.