5 Uliiweka nchi juu ya misingi yake,Isitikisike milele.
6 Uliifunika kwa vilindi kama kwa vazi,Maji yalikuwa yakisimama juu ya milima.
7 Kwa kukemea kwako yakakimbia,Kwa sauti ya radi yako yakaenda zake kasi,
8 Yakapanda milima, yakatelemka mabondeni,Mpaka mahali ulipoyatengenezea.
9 Umeweka mpaka yasiupite,Wala yasirudi kuifunikiza nchi.
10 Hupeleka chemchemi katika mabonde;Zapita kati ya milima;
11 Zamnywesha kila mnyama wa kondeni;Punda mwitu huzima kiu yao.